Pamoja na Jaja kuonyesha kiwango kizuri cha ufungaji kwa kuifungia Yanga mabao mawili katika mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC, Kocha wa Mtibwa Sugar, Mecky Maxime amesema wanataka pointi tatu dhidi ya kikosi cha Marcio Maximo.
Yanga inaanza Ligi Kuu bara ugenini dhidi ya Mtibwa Sugar Septemba 20. Maxime amesema wanajua Yanga moja ya timu zenye uwezo wa juu.
Lakini wamejipanga kuibuka na
ushindi katika mechi hiyo, akasisitiza anataka kumwonyesha Maximo kuwa na yeye ni
miongoni mwa makocha bora zaidi hapa nchini, japokuwa aliwahi kumfundisha soka.
Maximo aliwahi kumfundisha soka Maxime wakati
alipokuwa kocha mkuu wa timu ya soka ya taifa ‘Taifa Stars’ kuanzia mwaka 2006
hadi 2010.
“Pia nataka Maximo ambaye jina lake na langu tunatofautiana herufi
za mwisho ajue kijana wake hivi sasa nipo vizuri."
Mechi hiyo itapigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
0 COMMENTS:
Post a Comment