Kipa namba moja wa Simba, Ivo Mapunda,
amefunguka kuwa ameliona wazi pengo la aliyekuwa beki wa kati wa timu hiyo,
Donald Musoti kutokana na nafasi hiyo kupwaya.
Hivi karibuni uongozi wa Simba uliamua
kuachana na Musoti ili kumpisha mshambuliaji, Emmanuel Okwi, raia wa Uganda,
baada ya kufanikiwa kunasa saini yake akitokea Yanga.
Ivo amesema
kuna upungufu mkubwa katika nafasi ya beki ya kati kutokana na kukosekana kwa
Musoti.
“Tumecheza vizuri lakini pengo la Musoti
limeonekana sana na tutammisi, kwani ni mtu ambaye tulimzoea na alikuwa akitoa
ushirikiano wa hali ya juu.
“Ila hakuna tatizo kwa kuwa mabeki waliopo
wapo vizuri na nashukuru Mungu wananielewa vizuri pindi ninapowaelekeza uwanjani
na ninaamini tutafanya vyema kwenye ligi,” alisema Ivo.
0 COMMENTS:
Post a Comment