September 24, 2014

KOCHA MKUU COASTAL UNION, YUSUF CHIPPO
Timu ya Coastal Union ya jijini Tanga imeweka rekodi katika timu zote za ligi kuu kufuatia benchi lake la ufundi kuongonzwa na Wakenya tupu.
Coastal Union imeanza ligi kwa kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Simba ambapo kikosi chao kipo vizuri. Mabao yao yalifungwa na wageni Ramadhani Salim wa Kenya na Yayo Lutimba wa Uganda.
Wakenya hao walikuwa 'bize' wakiiongoza Coastal kwenye benchi la ufundi dhidi ya Simba.

Makocha hao ni  pamoja na kocha mkuu, Yusuf Chippo, kocha wa makipa, Razack  Siwa na kocha msaidizi, Benard Mwalala.
Benard aliwahi kuichezea Yanga kipindi cha nyuma ikiwa ni pamoja na kuichezea Coastal, huku Siwa akiwahi kuwa kocha wa makipa wa timu hiyo ya Yanga msimu wa 2012/13.


Timu hiyo ya Coastal imeonyesha kuja na kasi ya hali ya juu kwenye ligi ikiwa ni pamoja na kufanya mabadiliko ya kutosha kwa wachezaji wake licha ya walioitumikia msimu uliopita wengi wao kuondoka.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic