Kiungo mkabaji wa Simba, Mrundi, Pierre
Kwizera, amesifu usajili wa kiungo mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi na Mkenya
Paul Kiongera kwenye kikosi chao.
Wachezaji hao walijiunga na timu hiyo hivi
karibuni kwa ajili ya kuitumikia Simba kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu Bara
uliopangwa kuanza Septemba 20, mwaka huu.
Kwizera
alisema kuwa kabla ya kutua kwa washambuliaji hao, safu hiyo ya ushambuliaji,
haikuwa inafanya vizuri kutokana na kushindwa kutumia nafasi nyingi wanazozipata.
Kwizera alisema anaamini ujio wa wachezaji hao
utaimarisha safu hiyo ya ushambuliaji kutokana na uwezo wao mkubwa wa kufunga
mabao.
Aliongeza kuwa, wao kama viungo watafanya kazi
moja pekee ya kuwatengenezea pasi nzuri zitakazowafikia miguuni washambuliaji
hao kwa ajili ya kufunga mabao.
“Kiukweli kabisa ujio wa Okwi na Kiongera
umeimarisha safu ya ushambuliaji katika msimu ujao, kabla ya kuja washambuliaji
hao, timu ilikuwa inakosa nafasi nyingi za kufunga katika mechi za kirafiki.
“Lakini kutua kwao Simba, hakika kutaisaidia
sana timu yetu kutokana na uwezo mkubwa wa kufunga mabao,” alisema Kwizera.
0 COMMENTS:
Post a Comment