Mbeya City inayodhaminiwa na Betri za Magari za RB imepania kuendeleza kasi yake ya
msimu uliopita na ikiwezekana kupata zaidi ya nafasi ya tatu, Mbeya City
imejipanga kisawasawa.
Msimu uliopita, Mbeya City ilitumia mfumo wa
pasi fupifupi na kasi, hali ambayo ilileta ushindani wa hali ya juu kwenye ligi
na kufanya kila timu waliyokutana nayo kuhofia.
Ofisa Habari wa Mbeya City, Dismas Ten,
alifunguka kuwa, wanajipanga ipasavyo kuhakikisha wanaleta mabadiliko msimu
ujao kufuatia kocha kuamua kuachana na mfumo walioutumia msimu uliopita na
kuleta mpya pamoja na kuwa na mbinu mpya tofauti na zile zilizozoeleka.
“Msimu uliopita wachezaji walikuwa wakicheza
pasi fupifupi kwa kasi lakini safari hii kocha ameamua kuwabadilisha kwa
kuachana na mfumo huo na badala yake watatumia pasi ndefu na kwa kasi.
“Kocha anahitaji kuibadili timu ili iweze kuwa
katika kiwango kizuri na cha kiushindani zaidi msimu ujao tofauti na jinsi watu
walivyoizoea msimu uliopita, kwani kuna washambuliaji wazuri kama Deus Kaseke,
Paul Nonga na Mwagane Yeya,” alisema Ten.
0 COMMENTS:
Post a Comment