Baada ya kufanyiwa marekebisho kwa muda mrefu,
hatimaye Uwanja wa Kambarage katika Manispaa ya Shinyanga utakaotumiwa na Stand United msimu
ujao, umekamilika na kufungwa taa jambo ambalo litafanya michezo yake kuweza
hata kupigwa usiku.
Bodi ya Ligi hivi karibuni ilikamilisha ukaguzi
wa viwanja vyake ambavyo vitaanza kutumika rasmi Septemba 20, mwaka huu katika
Ligi Kuu Bara huku baadhi ya viwanja vikionekana kutokuwa bora kutokana na
kushindwa kukarabatiwa vema, vikiwemo viwanja vya Jamhuri Morogoro na Mkwakwani
Tanga.
Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Silas Mwakibinga,
amesema Uwanja wa Kambarage unaweza kutumiwa katika mechi za usiku kama itabidi
kwa kuwa taa zinaruhusu.
“Kambarage naweza kusema ni kiwanja bora
kilichorekebishwa vizuri kati ya viwanja vya mikoani vilivyofanyiwa
marekebisho, kimekuwa bora katika ‘pitch’ na taa ambazo zimefungwa,” alisema
Mwakibinga.
0 COMMENTS:
Post a Comment