Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amefunguka
kuhusiana na suala la mshambuliaji wake mpya Danny Welbeck kupoteza nafasi
katika mechi dhidi ya Borussia Dortmund.
Wenger amemkingia kifua Welbeck ambaye
alipoteza nafasi zaidi ya mbili katika yake ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya
akiwa na Arsenal.
Welbeck alinunuliwa na Arsenal kwa pauni
milioni 16 akitokea Manchester United.
Tokea jana usiku, amekuwa gumzo kwenye
mitandao wadau wakionyesha kuchukizwa naye kupoteza nafasi huku Arsenal
ikiambulia kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Wajerumani hao.
0 COMMENTS:
Post a Comment