Kocha Arsene Wenger, jana
alitumia muda wake mwingi kuzungumzia masuala ya ufundi huku akikumbushia
Arsenal inapokutana na timu za Kijerumani.
Wenger amewaeleza vijana
wake kuhusiana na nini cha kufanya kiufundi akiamini Borussia Dortmund si timu
ya lelemama.
Arsenal iko ugenini kuwavaa
Dortmund katika mechi ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mechi hiyo inatarajiwa kuwa
ngumu kutokana na ugumu wa wakali hao.
0 COMMENTS:
Post a Comment