Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard ametamba
kwamba wamerudi kazini kwenye Ligi Kuu ya Mabingwa Ulaya..
Mara ya mwisho Liverpool ilicheza michuano hiyo
mikubwa zaidi kwa ngazi ya klabu mwaka 2009.
Gerrard amesema alikuwa akiumia na kujisikia
vibaya lakini hakuwa na namna. Hivyo watafanya kila linalowezekana kufika
mbali.
Mara ya mwisho Liverpool ilitwaa kombe hilo mwaka
2005 katika mechi iliyopigwa Istambul Uturuki dhidi ya AC Milan ya Italia.
Gerrard amecheza mechi 129 za mechi za Ulaya zilizo
chini ya Shirikisho la Soka Tanzania (Uefa) wakati wachezaji wengine wote
waliobaki kwenye kikosi hicho ukijumlisha mechi zao za kimataifa wakiwa na
Liverpool zinafikia 153.
0 COMMENTS:
Post a Comment