MWOMBEKI AKIWASILI KIMYAKIMYA KWENYE UWANJA WA NDEGE WA JNIA JIJINI DAR KABLA YA KULIKWEA DEGE LA OMAN AIR KWENDA ZAKE KATIKA JIJI LA MUSCAT, LEO. |
Mshambuliaji wa zamani wa Simba, Betram MWombeki ameondoka
nchini leo kimyakimya kwenda nchini Oman inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza kufanya majaribio ya kucheza soka la
kulipwa.
Mwombeki ameondoka leo na kusema amejiandaa kwa ajili ya
majaribio.
“Nakwenda kufanya majaribio, kama nikifanikiwa, Oman Club
watafanya mazungumzo na Tanzania,” alisema.
Hata hivyo, Mwombeki hakutaka kufafanua zaidi na kusisitiza mambo
yakienda vizuri kila kitu kitakuwa hadharani.
0 COMMENTS:
Post a Comment