Uongozi wa klabu ya FC Lupopo ya DR Congo umesema umeamua
kulifikisha suala la madai yake kwa Yanga kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa
(Fifa).
Mmoja wa viongozi wa FC Lupopo aliyejitambulisha kwa jina moja
la Joseph amesema wameamua kwenda Fifa ili kuishitaki Yanga ambayo imeingia
mkataba na mchezaji wake Mbuyu Twite bila ya kuwalipa.
“Sisi tuna mkataba na Yanga, walimsajili Mbuyu kwa mkopo na wao
wanajua hili, lakini sasa wameongeza mkataba bila ya kutulipa.
“Tunataka tulipwe fedha zetu kwa kuwa mkataba wetu na Yanga uko
wazi, lakini wanatufanyia vitu si sahihi.
“Tumewasiliana nao, mwenzetu amefika hapo Dar es Salaam lakini
wamemzungusha tu bila ya mafanikio,” alisema na kuongeza.
“Tunaona Fifa wataamua kuhusiana na hilo, hatutazungumza tena na
Yanga,” alisema lakini alikataa kuweka wazi kipi walichokidai Fifa.
Hata hivyo, madai ya Lupopo yamekuwa yakichanganya kwa kuwa
Twite angecheza vipi miaka miwili kwa mkopo wakati walimnunua.
Pia imekuwa ikishangaza kama kweli Yanga ilimsajili Twite kwa
mkopo kwa kuwa ilielezwa ilimsajili moja kwa moja.
Hali hiyo tayari inaonekana kuanza kuzua hali ya sintofahamu
katika suala hilo na huenda kuna kitu kimejificha.
0 COMMENTS:
Post a Comment