Licha ya kushinda mabao 3-0, kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa, amefunguka
kuwa, Azam ilicheza vizuri zaidi yao katika mechi ya Ngao ya Jamii, Jumapili
iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa.
Ngassa amesema kuwa Azam walionyesha kiwango kikubwa
kipindi cha kwanza na Yanga walicheza kawaida sana.
Aliongeza
kuwa, tatizo lililosababisha wasifunge mabao kipindi cha kwanza ilitokana na
mshambuliaji wao, Mbrazili, Geilson Santana ‘Jaja’ kutotokea mapema kwenye
boksi kwa ajili ya kuunganisha krosi.
“Azam
walicheza vizuri sana tofauti na sisi ambao tulikuwa kawaida tu, hasa kipindi
cha kwanza kwa kuwa Jaja alikuwa akichelewa kuingia kwenye boksi la penalti la
wapinzani lakini tunashukuru tumeshinda bao hizo tatu,” alisema Ngassa na
kuongeza:
“Inaniuma
kwa kuwa sijafunga bao lolote licha ya kupata nafasi nyingi lakini ilinitokea
kwa bahati mbaya.”
Katika mechi hiyo, Yanga ilibanwa sana katika kipindi cha kwanza, lakini Azam FC wakashindwa kuzitumia nafasi walizozipata.
katika kipindi cha pili, ngoma ikabadilika na Yanga kutawala huku wakifanikiwa kupata mabao matatu yaliyoinyamazisha Azam FC.
0 COMMENTS:
Post a Comment