KISIGA (KATIKATI)... |
Zikiwa
bado siku chache ili kuanza kwa michuano ya Ligi Kuu Bara, kiungo mshambuliaji
wa Simba, Shabani Kisiga, amewapa somo zito wachezaji wenzake wa timu hiyo,
Emmanuel Okwi na Paul Kiongera kwa kuwataka kuachana na utani pindi wanapokuwa
uwanjani na badala yake wapambane mwanzo mwisho.
Kisiga
ambaye amejiunga na Simba hivi karibuni akitokea Mtibwa Sugar, amesema kuwa,
Okwi, Kiongera pamoja na yeye mwenyewe, kwa sasa ndiyo wachezaji wa klabu hiyo
wanaotupiwa macho na mashabiki, hivyo wanatakiwa kufanya kazi kikweli.
Kikosi
cha Simba kwa misimu miwili mfululizo, kilishindwa kufanya vizuri katika
michuano ya ligi kuu na kujikuta kikikosa nafasi ya kuiwakilisha nchi katika
michuano ya kimataifa.
“Tuna
kazi kubwa ya kufanya safari hii, hivyo utani hautakiwi kabisa uwanjani, kila
mchezaji anatakiwa kupambana kwa nguvu zake zote ili aibu ambayo timu hii
imeipata miaka iliyopita isitokee tena.
“Hata hivyo, wachezaji ambao wanatakiwa
kuwa makini zaidi ni wale tuliojiunga na Simba hivi karibuni kwa sababu macho
na masikio ya mashabiki wa timu yapo kwetu,” alisema Kisiga.
0 COMMENTS:
Post a Comment