Baada ya kuwapiga stop washambuliaji wawili wa Simba, Idara ya Uhamiaji Tanzania, sasa imesema hata Kocha Patrick Phiri wa Simba, pia hatakiwi kufanya kazi.
Idara ya Uhamiaji imesema Phiri raia wa Zambia hana kibali cha kufanya kazi nchini na wala klabu yake haijaomba.
Lakini ikasisitiza kwamba watani wao Yanga, tayari wameomba vibali vya Wabrazil wanne ambao ni Makocha, Marcio Maximo na msaidizi wake Leonaldo Leiva pamoja na mshambuliaji Jaja na Coutinho.
Uhamiaji kupitia Naibu Kamishna wake Abbas Irovya imesisitiza, Phiri naye asikae kwenye benchi wala kuifundisha Simba.
Simba inashuka dimbani Jumamosi kuivaa Polisi Moro kwenye Uwanja wa Taifa, hivyo lazima juhudi zifanyike kupata kibali leo na kesho, kama itashindikana basi kocha huyo hatakaa kwenye benchi.
Tayari Idara ya Uhamiaji imewazuia wachezaji Paul Kiongera raia wa
Kenya na Emmanuel Okwi kutoka Uganda kwa kuwa hawana vibali na hakuna maombi yaliyowasilishwa kuomba.
0 COMMENTS:
Post a Comment