Uongozi wa klabu ya Simba
umesema sare ya mabao 2-2 dhidi ya Coastal Union, jana, haukuwa mzuri kwao
lakini wameupokea kama changamoto.
Makamu wa Rais wa Simba,
Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesema wanaichukulia sare hiyo kama changamoto na
sehemu ya kujipanga.
KABURU. |
“Hakuna aliyetarajia,
inawezekana vijana wetu walijisahau baada ya kuongoza kwa mabao mawili wakaona
tumeshinda.
“Kipindi cha pili Coastal
Union wakajirekebisha na kucheza mchezo mzuri na kutupa wakati mgumu, mwisho
wakasawazisha,” alisema Kaburu.
“Tayari tumeanza kambi
Zanzibar na tutayatumia makosa ya mechi iliyopita kama sehemu kujiimarisha.”
Simba itacheza mechi ya
pili dhidi ya Polisi Morogoro katika mechi itakayopigwa Jumamosi ijayo.
0 COMMENTS:
Post a Comment