Kocha
wa timu ya OFI ya Ligi Kuu Ugiriki, Gennaro Gatuso ameshindwa kuonyesha
uvumilivu kwenye mkutano wa waandishi na kuanza kuporomosha matusi.
Gatuso,
kiungo mkorofi wa zamani wa AC Milan, alianza kuporomosha matusi kutokana na
kuzidiwa maswali.
Timu
yake iko katika nafasi ya nane katika msimamo wa ligi baada ya kushinda mechi
mbili, imepoteza mbili na Gatuso amekuwa hana raha.
Gatuso
,36, aliuliza kutokana na mwenendo mbaya wa timu yake ambayo inaelezwa kutokuwa
katika hali nzuri ya kiuchumi.
Alisema:
“OFI sio Real Madrid, sio Barcelona. Ninataka wachezaji wangu kucheza kwa
kujituma, tena kwa moyo.
“Sitaki
visingizio eti klabu haina mshahara (tusi)," akiinua kidole cha kati kuonyesha ishara ya tusi kulielekeza upande wa waandishi.
“Kwa
waandishi pia mmekuwa mkiandika eti naondoka, naondoka wapi, nani kawaambia,
sijaja hapa kwa ajili ya kula raha.
0 COMMENTS:
Post a Comment