Mashabiki wa soka nchini Ureno wamechangia kwenye mitandao
mbalimbali wakionyesha kusikitishwa na ugomvi wa nyota wao wawili.
Kocha Jose Mourinho wa Chelsea na mshambulia Cristiano Ronaldo wa
Real Madrid wameeleza hadharani kuwa hawana urafiki tena.
Mashabiki hao wa soka wameeleza wazi kusikitishwa na hali hiyo
huku wakishindwa kugawanyika wampede nani.
Baadhi wamesema Ureno yenye watu milioni 11 na nyota wachache
wanaojulikana zaidi duniani kama hao wawili, hivyo hawakupaswa kuwa maadui.
Kauli ya Mourinho kwamba walitolewa kwenye nusu fainali ya Ligi ya
Mabingwa mwaka 2012 baada ya Ronaldo kukosa penalti na limekuwa jambo ambalo
linamuumiza kila mara ilioonyesha kumuudhi mshambuliaji huyo.
Ronaldo alijibu mashambulizi kwa kusema hayuko katika soka
kutafuta marafiki na hiyo ilikuwa baada ya kuulizwa kama uhusiano wake na
Mourinho ni mzuri.
Wawili hao walifanya kazi pamoja Real Madrid tokea mwaka 2010 hadi
2012 Mourinho alipoondoka na kwa mambo yanavyokwenda inaonekana uhusiano wao
haupo.
“Urafiki wetu haupo, ulishakufa, si lahisi kutuona tukiwa pamoja,”
Mourinho aliiambia moja ya runinga marufu ya Ureno wakati akifanyiwa mahojiano.
0 COMMENTS:
Post a Comment