Na Saleh Ally
LIGI Kuu Bara inaanza leo,
hakuna ubishi kati ya binadamu walio kwenye presha ya juu ni makocha wakuu 14
wanaoshiriki ligi hiyo.
Hauwezi ukasema kuna kila
kocha atakuwa anataka kombe, wako wanaamini kuwa kuna ugumu lakini kila mmoja
atajaribu ili alipate.
Kuna madaraja mawili katika
mioyo au malengo ya makocha hao. Kwanza ni kulipata kombe hilo na kushiriki
michuano ya kimataifa, hizo ni nafasi mbili, ya kwanza na ile ya pili.
Ikishindikana ni mpango wa
pili, kubaki Ligi Kuu Bara ili msimu mwingine waendelee kujaribu kupambana
kubeba kombe, kushiriki michuano ya kimataifa au kubaki.
Kwa makocha hao wa timu 14,
kivutio ni hivi, kati yao wenyeji ni nane na sita waliobaki ni wageni ambao
wanatokea katika nchi tano.
Kenya ina makocha wawili
ambao wanazinoa Coastal Union na Ruvu Shooting, halafu wageni wengine wanne ni
kutoka Zambia-Patrick Phiri wa Simba, Brazil, Marcio Maximo (Yanga),
Cameroon-Patrick Omog (Azam FC) na Uganda-Jackson Mayanja (Kagera).
Makocha hao sita wa kigeni wanapambana wao kwa wao halafu
dhidi ya wenyeji wakati wenyeji wanapambana dhidi ya wageni.
Kombe litachukuliwa na
wazalendo wanane au lazima litakwenda nje. Maana makocha wageni wamekuwa
wakitawala.
Kuna mwenyeji anaweza
kupambana nao, Juma Mwambusi wa Mbeya City alionyesha njia na kushika nafasi ya
tatu msimu uliopita. Vipi kuhusu msimu huu?
Kama yeye akishindwa, mwali
atakwenda Brazil iwapo watamchukua Yanga, Zambia kama ataenda Simba au atabaki
Cameroon kwa Omog ndani ya Azam FC?
Lakini kuna Wakenya wawili
na Mganda mmoja ambao pia watakuwa wanapambana. Maswali ni mengi lakini majibu
yanaanza leo.
MABOSI 14 LIGI:
Yanga – Marcio Maximo
(Brazil)
Ndanda FC- Denis Kitambi
(Tanzania)
Polisi Moro- Aldoph Rishard
(Tanzania)
Stand United- Emmanuel
Masawe (Tanzania)
Mbeya City- Juma Mwambusi
(Tanzania)
Azam FC- Joseph Omog
(Cameroon)
Simba- Patrick Phiri
(Zambia)
JKT Ruvu- Fred Felix
Minziro (Tanzania)
Mtibwa Sugar- Mecky Maxime
(Tanzania)
Ruvu Shooting- Tom Olaba
(Kenya)
Prisons – David Mwamwaja (Tanzania)
Mgambo- Bakari Shime
(Tanzania)
Coastal Union- Yusuf Chippo
(Kenya)
Kagera Sugar-Jackson
Mayanja (Uganda)
FIN.
Viwanja vilivyorejea ligi
kuu..
INGAWA zimepanda timu tatu
kwenye Ligi Kuu Bara, mbili zikiwa ‘mpya’ kabisa, ni viwanja viwili tu ndiyo
vitakuwa vimerejea kwenye ligi hiyo.
Kambarage Shinyanga ambao
utatumiwa na
Kagera-Kaitaba
Ndanda-Nangwanda
Stand-Kambarage
Yanga, Simba-Taifa
Mtibwa, Polisi-Jamhuri
Prisons, Mbeya City-
Sokoine
Azam FC- Chamazi
JKT Ruvu, Ruvu-Mabatini
Coastal, Mgambo- Mkwakwani
0 COMMENTS:
Post a Comment