Na Mwandishi Wetu
HAKUNA anayeweza kukataa kwamba timu tatu au
nne zitakazokuwa na msimu mgumu zaidi kwenye Ligi Kuu Bara, Azam FC na Mbeya
City zitaongoza.
Simba inaweza kuwa moja ya timu hizo kwa
kuwa inataka kujinyanyua na kurejea kwenye daraja la heshima yake.
Lakini Azam FC na Mbeya City ndiyo wenye
kazi ngumu zaidi kwa kuwa msimu wao wa kwanza wa ligi kuu wakamaliza wakiwa
katika nafasi ya tatu.
Hakuna timu ambayo itakwenda kucheza dhidi
ya Mbeya City ikiwa ‘ime-relax’ kwa kuwa inajua ni kibarua kigumu.
Pia hakuna timu itataka kugeuzwa sehemu ya
njia ya mafanikio ya Mbeya City kwa mara ya pili mfululizo.
Wao Mbeya City ambao wanadhaminiwa na
kampuni ya Bin Slum Tyres ambayo inatangaza betri zake za RB, imeanza maandalizi
ikijua msimu huu utakuwa mgumu kwao.
Timu chini ya Kocha Juma Mwambusi imeanza
maandalizi na hadi jana ilikuwa imejichimbia nje ya jiji la Mbeya. Hii
inaonyesha kiasi gani wamepania kuendeleza walichokianzisha msimu uliopita.
Deni lao ni kwamba, katika msimu wa kwanza
wa ligi kuu. Mbeya City chini ya kocha Mzalendo, Mwambusi ilifanikiwa kufikisha
pointi 48, si mchezo.
Kumbuka, Simba iliyoshika nafasi ya nne
ilikuwa na pointi 38, tofauti ya pointi 11 dhidi ya Mbeya City.
Kwa hesabu za kawaida, ili Mbeya City
ifanikiwa, lazima iwe na uhakika wa kufikisha pointi hizo, halafu na zaidi.
Japo wingi au uchache wa pointi, pia unaweza kupunguzwa au kuongezwa kutokana
na ugumu au ulaini wa ligi.
Azam FC:
Hawa ndiyo mabingwa waliositisha utawala wa
Simba kwa zaidi ya miaka 10. Lakini ndani ya miaka 25 Mtibwa Sugar pekee
iliingia katika ya wakongwe Yanga na Simba na kutwaa kombe baada ya Coastal
Union mwaka 1988 na baadaye Mtibwa Sugar mara mbili.
Mtibwa Sugar pekee walifanikiwa kutwaa mara
mbili mfululizo dhidi ya wakongwe hao. Azam FC wataweza?
Maana wakongwe pia ni wabishi na safari hii
wana vikosi imara. Wanataka kurudisha heshima na hawatakuwa tayari kuendelea
kulikosa kombe.
Azam FC ilifikisha pointi 62 zilizoiewezesha
kutwaa ubingwa msimu uliopita ikiwa ni ongezeko la point inane tu ukilinganisha
na msimu wa 2012-13 ambao Yanga ilikuwa bingwa na pointi 60.
Azam FC inaweza kujiongeza, haina kikosi
kinachobadilika sana, lakini Yanga katika misimu miwili imekuwa bingwa na
nafasi ya pili.
Simba ndiyo ina deni kubwa, misimu yote
miwili haijabeba ubingwa na imeshika nafasi ya tatu na nne. Sasa inataka
kurudi.
Hii ndiyo picha halisi ya ushindani hata
kabla ya kuanza kwa ligi na ukiangalia katika timu hizi nne, Yanga, Simba, Azam
FC na Mbeya City, yupi atashika mbili bora.
Je, kati ya Polisi Moro, Stand United na
Ndanda FC, kati yao kuna mgeni ataingia kati kama walivyofanya Mbeya City msimu
wa kwanza?
Tano Bora ya misimu miwili…
2013/2014
P W D L F A GD PTS
1. Azam 26 18 8 0 51 15 36 62
2. Yanga 26 16 8 2 61 19 42 56
3. Mbeya 26 13 10 3 32 19 13 49
4. Simba 26 9 11 6 41 27 14 38
5. Ruvu 26 10 8 8 28 32 -4 38
2012/2013
P W D
L F
A GD PTS
1. Yanga 26 18 6 2 47 14 33 60
2. Azam 26 16 6 4 46 20 26 54
3. Simba 26 12 9 5 38 25 13 45
4. Kagera 26 12 8 6 27 19 8 44
5. Mtibwa 26 10 9 7 29 25 4 39
0 COMMENTS:
Post a Comment