Klabu kongwe nchini ya Yanga, imeingia mkataba
wa kudumu na Benki maarufu nchini ya CRDB.
CRDB ndiyo itakayofanya kazi ya kutengeneza
kadi za wanachama wa Yanga ambao watakuwa wakikatwa ada zao moja kwa moja.
Maana yake sasa, benki ya Posta imebaki na watani wa Yanga, Simba ambao wanaendelea nayo.
Lakini leo wakati wa uingiaji mkataba ulioongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Yanga, Mama Fatma Karume na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa CRDB, Charles Kimei, suala la TPB halikutakiwa kugusiwa.
Lakini leo wakati wa uingiaji mkataba ulioongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Yanga, Mama Fatma Karume na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa CRDB, Charles Kimei, suala la TPB halikutakiwa kugusiwa.
Kimei amesema kuwa makubaliano hayo waliyoingia
siyo ya kushindana na benki nyingine yoyote kikubwa ni kuwafikia wanachama
karibu.
Kimei alisema, wanachama wa timu hiyo
wanatakiwa kuchangia kiasi cha shilingi 8000 kwa ajili ya kufungulia akaunti
huku kadi ikitolewa bure bila ya malipo yoyote.
“Sisi
tutakuwa tayari kuwapa nafasi hata wale wenye klabu nyingine, lakini kwa kuwa
tumeingia mkataba na Yanga, tunawapa kipaumbele zaidi,” alisema Kimei.
“Mkataba
wetu hauna kikomo ni wa muda mrefu, wao au sisi mmoja wao kama hasiporidhishwa
na huduma ya mwenzake, atasitisha mkataba,”alisema Kimei.
Kuhusiana na mkataba huo alioingia mbele ya
waandishi, Mama Karume alisema
kuwa wanaamini utakuwa na mafanikio makubwa.
“Tunaishukuru
benki ya CRDB ya kuingia mkataba na Yanga huu wa utengenezaji wa kadi za
uanachama huku tukipata huduma za kibenki.
“Nafikiri hiyo ni kutokana na uongozi bora
wenye busara uliokuwepo madarakani, Yanga hivi sasa ni klabu kubwa yenye
kiwango cha kimataifa, hivyo inahitaji kupata wadhamini zaidi ya hapa
ilipofikia,”alisema Karume.
CRDB ni kati ya benki kubwa zaidi nchini
zilizosambaa nchi nzima, hali ambayo itaisaidia Yanga kupata wanachama kwa
wingi zaidi.
0 COMMENTS:
Post a Comment