Vigogo wa Kenya, Gor Mahia wanakuja nchini
kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Simba, Jumamosi.
Simba watawavaa Wakenya hao Jumamosi kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ikiwa ni mechi ya kwanza ya Kocha Patrick
Phiri kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Phiri ameiongoza Simba kushinda mechi tatu za
kirafiki lakini hajacheza hata mechi moja ya kimataifa wala kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar.
Gor Mahia ambao waliwahi kufundishwa na Kocha
wa zamani wa Simba, Zdravko Logarusic na baadaye Bobby Williamson ambaye sasa
ni Kocha wa Harambee Stars, ni moja ya vikosi imara vya Kenya.
0 COMMENTS:
Post a Comment