Kocha wa Yanga, Marcio Maximo raia wa Brazil
alishindwa kuficha mapenzi yake kwa kipa wa Simba, Ivo Mapunda.
Wawili hao walifanya kazi katika kikosi cha
Taifa Stars na kwa mara ya kwanza walikutana tena uwanjani mara baada ya suluhu
Yanga na Simba zilipokutana wiki iliyopita.
Maximo alitumia takribani dakika moja na nusu
kumkumbatia na baadaye kuzungumza na Ivo huku sura yake ikionyesha mapenzi ya
dhati kwa kipa huyo wa zamani wa Yanga na Taifa Stars..
0 COMMENTS:
Post a Comment