Kipa kinda wa Simba, Peter Manyika amesema alidaka mechi dhidi ya Yanga kwa presha kubwa ya
kutokufungwa kwa kuhofia Baba yake mzazi, Manyika Peter kuhusishwa kama
angekosea na kuruhusu bao.
Kinda huyo, alidaka mechi
hiyo ikiwa ya kwanza kwenye msimu huu wa Ligi Kuu Bara tangu ajiunge na timu
hiyo iliyocheza michezo minne na kutoka sare yote.
MANYIKA PETER, BABA MZAZI WA PETER MANYIKA. HAPA ALIKUWA KAZINI NCHINI OMAN AMBAKO NI KIPA WA MAKIPA WA KIKOSI CHA SEEB. |
Alipata nafasi hiyo ya
kudaka baada ya makipa wakongwe wa timu hiyo kupata majeraha kwenye sehemu
mbalimbali.
Manyika amesema kuwa kabla ya mechi hiyo mashabiki wengi wa Simba
hawakuwa na imani naye wakihofia huenda akafungisha, lakini anashukuru
hakufungwa.
“Nilicheza mechi ya Yanga nikiwa na presha kubwa ya kupoteza
mechi ile, kwa sababu nilihofia kufungwa na baadaye kutajwa baba yangu ndiyo
chanzo kutokana kuwahi kuidakia timu hiyo.
“Lakini ninashukuru sikuruhusu bao katika mechi hiyo dhidi ya
Yanga, kikubwa mashabiki wanatakiwa kujenga imani na mimi nikiwa golini tukiwa tunacheza na Yanga,” alisema
Manyika.
0 COMMENTS:
Post a Comment