BALOTELLI AKIWA NA MPENZI WAKE, FANNY NAGUESHA. |
Mshambuliaji wa Liverpool, Mario Balotelli amefunguka
na kusema sasa amekua, wasimlinganishe na ilivyokuwa awali.
Balotelli raia wa Italia mwenye asili ya
Ghana amesema wanaodhani hufanya tendo la ndoa siku ya mechi, wanajichekesha
wenyewe.
Mshambuliaji huyo mwenye vituko amesema
hawezi kufanya tendo la mapenzi wakati anajua ana mechi.
“Kila mtu amefanya makosa katika wakati
anajua, mimi pia nimekua hivyo. Lakini usifikiri leo nitafanya mapenzi saa tatu
kabla ya mechi.
“Nimekua, kuna makosa ninayajutia lakini
tatizo England vyombo vya habari vinaandika mabaya ya Balotelli tu.
“Hazijali, zinaniona kama tatizo na
inawezekana watu wananiona tatizo kwa kuwa vyombo vya habari vinaripoti hivyo.
“Wako hadi wanaosahau kuhusiana na mpira
wangu na wanaamini mimi ni tatizo kwa kuwa vyombo vya habari ndivyo vinaripoti
hivyo.
“Wanachotakiwa kujua sasa nimekua,
ninakwenda ninabadilika na sitakuwa yule wa awali,” alisema Balotelli.
0 COMMENTS:
Post a Comment