October 17, 2014



Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Andrey Coutinho anaonekana yuko fiti kweli, ikiwezekana mabeki wa Simba wanatakiwa kuwa makini.

Raia huyo wa Brazil amekuwa akiwapa wakati mvumu mabeki wa Yanga na hasa wale ngangari kama Nadir Harob ‘Cannavaro’ na Kelvin Yondani.

Pamoja na kuwa imara lakini Cannavaro na Yondani walilazimika kufanya kazi ya ziada kumzuia.
Mara kadhaa walilazimika kumkumbatia au kumfanyia madhambi kutokana na ujanja wake.

Mabeki wa Simba watakuwa na kazi ya kumzuia kesho Jumamosi wakati watani hao watakapokutana.
Kocha Marcio Maximo amekuwa akimpanga ili apambane na mabeki imara kama Cannavaro na Yondani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic