Kocha Marcio Maximo amekuwa akimtumia zaidi mshambuliaji Hussein Javu katika mazoezi ya kikosi chake.
Maximo alikuwa akimuelekeza Javu namna ya kuiwahi mipira inayopigwa katikati ya uwanja.
Pia Javu amekuwa akipigiwa pasi na kukimbia kasi akikatiza katikati ya uwanja.
Huenda Maximo alikuwa akitengeneza mfumo maalum kama plan B.
Na inaonekana atamtumia Javu katika mechi yao dhidi ya watani Simba, kesho na huenda ataingia kipindi cha pili.
0 COMMENTS:
Post a Comment