October 24, 2014

CHID BENZ
Msanii maarufu wa Hip Hop nchini, Chid Benz ameshikwa akiwa na bangi na madawa ya kulevya.

Chid Benz ambaye jina lake halisi ni Rashidi Abdallah Makwiro, ameshikwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Habari za ndani zimeeleza Chid Benz ameshikwa akiwa na kete 12 za madawa aina ya heroine wakati akiwa njiani kwenda kufanya shoo mjini Mbeya.
Shoo hiyo ya Instagram Party ilipangwa kufanyika kesho mjini Mbeya.
Kamanda wa Kuthibiti na kupambana na Madawa ya Kulevya, Godfrey Nzowa amethibitisha kukamatwa kwa Chid Benz.
“Kweli tumemkamata bwana Rashidi Makwiro maarufu kama Chid Benz akiwa na kete kumi na mbili pamoja na misokoto ya bangi.
“Tunamshikilia kwa mahojiano maalum, lakini hauwezi kueleza sehemu alipo kwa sasa,” alisema Nzowa.
Chid Benz ni kiongozi wa kundi la La Familia lenye makazi yake Ilala jijini Dar.



1 COMMENTS:

  1. Msanii mpumbavu hafai hata kuonewa huruma. Tabia kama hizi ni lazima zipingwe kwa nguvu zote

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic