Ni furaha kubwa kwa mashabiki wa Simba, baada
ya wachezaji wake Emmanuel Okwi na Jonas Mkude kufanya mazoezi jioni hii mjini
Mbeya.
Okwi amefanya mazoezi kwenye kikosi cha timu
hiyo ambacho kimetua hapo kuivaa Prisons wikiendi.
Awali daktari wa Simba, Yassin Gembe alisema
asubuhi Okwi alishindwa kufanya mazoezi.
“Jioni hii Okwi amefanya mazoezi, asubuhi
ilikuwa kidogo ana tatizo la enka. Alikimbia lakini baadaye akalazimika kidogo
kusubiri nje.
“Ila jioni hii amefanya mazoezi vizuri sambamba
na wenzake. Pia Mkude ameanza mazoezi,” alisema Gembe.
Tayari Simba imecheza mechi nne kwenye Uwanja
wa Taifa jijini Dar es Salaam na zote imetoka sare.
0 COMMENTS:
Post a Comment