SONO (KULIA) AKIZUNGUMZA NA VIONGOZI WA SIMBAPAMOJA NA MABOSI WA BENCHI LA UFUNDI NYUMBANI KWAKE LEO SAA 2 USIKU. |
Uongozi wa
Simba umetua nyumbani kwa milionea wa soka nchini Afrika Kusini, Ephraim
Matsilela Sono.
Sono marufu
kama Jomo Sono, Braa J au Black Prince of South Africa Soccer ndiye mmiliki wa
klabu kongwe na maarufu ya Jomo Cosmos.
Viongozi hao
wa Simba wakiongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Mohammed Nassor ‘Kigoma’,
Said Tully, Kocha Patrick Phiri na Msaidizi wake, Selemani Matola walimtembelea
milionea huyo nyumbani kwake katika eneo la Hyghton jijini Johanesburg.
Sono amewahi
kuwa mwanasoka aliyeng’ara akiwa na Orlando Pirates kabla ya kununua klabu yake
akiwa ndiyo amerejea kutokea nchini Marekani alikokuwa akiishi na kucheza soka.
Amewahi kuwa
kocha wa timu kadhaa za Afrika Kusini pia amewahi kuwa Kocha Mkuu wa
Bafanabafana na ikapata mafanikio makubwa.
Sono amewahi
kufanya kazi nyingi zaidi kwa wakati mmoja, akiwa mmiliki wa Jomo Cosmos,
lakini kocha na mkurugenzi wa ufundi, pia bosi wa usakaji vipaji kwa watoto.
Hata hivyo
haikuelezwa Simba walifika nyumbani kwake kumtembelea au kuanzisha uhusiano wa
kibiashara kati ya klabu hizo mbili, yaani Simba na Jomo Cosmos ambayo
anaimiliki.
0 COMMENTS:
Post a Comment