Kiingilio
cha mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kati
ya Tanzania (Taifa Stars) na Benin (Squirrels) itakayochezwa Jumapili Oktoba 12
mwaka huu jijini Dar es Salaam ni sh. 4,000.
Washabiki
watakaolipa kiingilio hicho katika mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Taifa ni
kwa ajili ya viti vya rangi ya chungwa, kijani na bluu. Kwa washabiki
watakaokaa jukwaa la VIP B kiingilio ni sh. 10,000. Tiketi kwa ajili ya mechi
hiyo ni za elektroniki ni
Viti
vya VIP A na C hakutakuwa na viingilio, na badala yake vitatumika kwa ajili ya
wageni maalumu watakaolikwa kutoka katika madhehebu ya dini za Kikristo na
Kiislamu.
Mechi
kati ya Taifa Stars na Squirrels itaanza saa 11 kamili jioni, na itatanguliwa
na mechi ya kudumisha upendo, amani, udugu na ushirikiano kati ya timu za
taasisi za dini ya Kiislamu na Kikristo itakayochezwa kuanzia saa 9 kamili
alasiri.
Wakati
huo huo, Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imeingia
kambini leo (Oktoba 6 mwaka huu) kwenye hoteli ya Accomondia jijini Dar es
Salaam tayari kwa mechi dhidi ya Benin.
Timu
hiyo chini ya Kocha Mart Nooij kesho (Oktoba 7 mwaka huu), Jumatano (Oktoba 8
mwaka huu) na Ijumaa (Oktoba 10 mwaka huu) saa 10 jioni itafanya mazoezi Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam.
Mshambuliaji
Thomas Ulimwengu kutoka timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo
(RDC) na kiungo Mwinyi Kazimoto kutoka timu ya Al Markhiya ya Qatar tayari
wametua nchini kujiunga na kikosi cha Taifa Stars.
Naye
mshambuliaji Juma Liuzio kutoka timu ya Zesco ya Zambia anawasili nchini kesho
(Oktoba 7 mwaka huu) mchana kwa ndege ya Kenya Airways akitokea Ndola kupitia
Nairobi.
ajili
ya mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 11 jioni.
Kwa
mujibu wa Kocha Nooij, timu hiyo itakuwa na vipindi (sessions) 11 vya mazoezi
kabla ya kucheza na Benin (Squirrels). Stars itafanya mazoezi asubuhi na jioni
kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa ambapo baadhi yatafanyika Uwanja wa Taifa, na
mengine kwenye uwanja mwingine.
Wachezaji
Thomas Ulimwengu na Mbwana Samata wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo (DRC) pamoja na Mwinyi Kazimoto anayechezea timu ya Al
Markhiya ya Qatar wanawasili nchini kesho (Oktoba 6 mwaka huu).
0 COMMENTS:
Post a Comment