Mshambuliaji Juma Liuzio anayechezea timu ya Zesco ya Zambia atawasili nchini keshokutwa (Oktoba 7 mwaka huu) kwa ndege ya Kenya Airways akitokea Ndola.
Luizio ambaye aliwahi kukipiga Mtibwa Sugar, pia aliwahi kufanya majaribio nchini Afrika Kusini kabla ya kupata nafasi Zambia.
Mshambuliaji huyo, ameitwa na Kocha Mart Nooij kwa mara ya kwanza na atakuwa akigombea namba na washambuliaji wawili nyota, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaokipiga TP Mazembe ya DR Congo.
0 COMMENTS:
Post a Comment