Homa ya mechi ya Simba na Yanga ya Ligi Kuu
Bara ambayo itapigwa Oktoba 18, mwaka huu imezidi kuteka hisia za mashabiki
wengi ambapo sasa imefahamika kuwa tiketi zitaanza kuuzwa siku sita kabla ya
mechi.
Ofisa Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Silas
Mwakibinga, amesema licha ya maneno
ya hapa na pale juu ya matumizi ya teknolojia ya kununua tiketi kwa
elektroniki, bado wataendelea na mfumo huo huku ulinzi ukiimarishwa zaidi siku
ya mechi.
“Tumekubaliana tuanze kuuza tiketi Oktoba 13,
pia suala la ulinzi, tunatarajia kuwa na askari zaidi ya 400 siku hiyo,”
alisema Mwakibinga.
0 COMMENTS:
Post a Comment