MUSOTI WAKATI AKIWA MAZOEZINI SIMBA. KULIA NI SHABANI KISIGA. |
Hatimaye Klabu ya Simba imeonyesha kukubali
kukaa meza moja na beki Donald Musoti ili kumalizana kwa kilichotokea wiki
chache zilizopita, lakini beki huyo raia wa Kenya ameweka ngumu.
Rais wa Simba, Evans Aveva, amesema kuwa wao wapo tayari kukaa na Musoti meza moja ili kuweza
kulimaliza lakini majibu waliyoyapata kutoka kwa beki huyo ni kuwa yeye hawezi
kuzungumza kwa sasa.
“Musoti bado tunamtambua kuwa ni mchezaji wetu
halali kwani bado ana mkataba na Simba, kuhusu suala lake hadi sasa bado
linaendelea na hatujapata muafaka, awali tulimwita ili kuweza kumalizana naye
lakini alikataa kwa madai kuwa tayari suala hilo ameshalifikisha kwa wakala wake
na ndiye mtu tunayetakiwa kufanya naye mazungumzo.
“Kitu kinachotutatiza ni kwamba wakala wake pia
ni mgeni, hivyo inakuwa tatizo kumpata lakini kuhusu barua ya Fifa ambayo
amedai wanataka kutupatia bado hatujaipata na tunasubiri tuipate ili kuweza kuona
kile kilichojili na kutoa majibu kulingana na kile kilichoandikwa,” alisema
Aveva na kuongeza:
“Sisi tulikuwa radhi kuendelea naye lakini
aliondoka bila ya kutoa taarifa kwa uongozi hivyo ikawa vigumu kukutana naye,
tunasubiria barua ili kuweza kukaa naye meza moja na kulimaliza tatizo hili.”
Simba ilimuondoa Musoti dakika za mwisho kwenye
majina yake ya usajili na kumuingiza Emmanuel Okwi, mchezaji huyo alilalamika
kutotendewa haki na inaelezwa amefikia makubaliano ya kuichezea Tusker ya
Kenya.
0 COMMENTS:
Post a Comment