Kipa Ivo Mapunda ndiye
atakaekaa langoni katika mechi dhidi ya Yanga, keshokutwa.
Tayari Ivo ambaye alijiunga
na Simba nchini Afrika Kusini na kufanya mazoezi kwa siku mbili, amesema yuko
fiti.
Vipimo alivyofanyiwa Afrika
Kusini kupata uhakika katika kidole alichovunjika.
“Sasa kila kitu safi, Ivo
atakaa langoni na nafasi kipa wa pili atakuwa Manyika.
“Hivyo anaendelea na
mazoezi na ndani ya leo na kesho atakuwa safi,” kilieleza chanzo.
Kipa Hussein Shariff ‘Cassilas’
naye ni majeruhi.
Tayari Simba imerejea
jijini Dar es Salaam na kuendelea na mazoezi.
0 COMMENTS:
Post a Comment