Mshambuliaji wa Liverpool, Raheem
Sterling ameendelea kushambuliwa kutokana na kitendo chake chake cha kusema
amechoka kuichezea England katika mechi yake ya kimataifa.
Kilichowaudhi zaidi
mashabiki ni kumuona akiendesha gari mwenyewe kwenda mazoezini Liverpool.
Mashabiki hao walianza
kumshambulia kwenye mtandao wa Twitter wakidai alidanganya.
Wengi wamekuwa wakisema
kitendo chake cha kudai amechoka ni kuonyesha kiasi gani si mzalendo.
Wako baadhi wamekuwa
wakiponda uamuzi huo na kudai umetoakana kutokuwa na asili ya England kwa
asilimia mia. Mshambuliaji huyo ana asili ya Jamaica.
0 COMMENTS:
Post a Comment