![]() |
| COASTAL UNION IKIPAMBANA NA SIMBA WAKATI IKITUMIA JEZI ZENYE UDHAMINI WA SOUND MSIMU ULIOPITA. |
Makamu Mwenyekiti wa Coastal Union, Steven Mguto ameonyesha
kubabaika kuhusiana na uamuzi wa klabu hiyo kutaka kuifungulia mashitaka
kampuni ya Bin Slum Tyres Ltd.
Mguto amesema suala hilo lilijitokeza kwenye kikao chao cha kamati
ya utendaji, lakini lilikuwa wazo la mjumbe mmoja tu.
| MGUTO (KULIA) AKIWA NA MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI YA COASTAL UNION, SALIM AMIR. |
Akihojiwa na Redio One jana, Mguto alionekana kubabaika baada ya
kuulizwa kama aliona ni sahihi wao kufungua mashitaka.
“Kwa kweli naomba tuliache, maana ni suala ambalo lilikuwa ni wazo
la mjumbe mmoja tu kwenye kikao.
“Nashindwa kusema sawa au la, lakini acha kwanza tusubiri,”
alisema.
Alipoulizwa kuwa, kama sasa wanashinikiza mashabiki wa Coastal
Union kutovaa jezi za zenye nembo ya mdhamini Sound, msimu ujao wakiachana na
mdhamini wa sasa Pembe, watawazuia tena mashabiki kutovaa?
“Kwa kweli hapo una hoja ya msingi, ndiyo maana nakuambia tuliache
kwanza suala hilo kwa sasa,” alisema Mguto.
Sakata hilo limezidi kupaa baada ya uongozi wa Coastal Union
kushinikiza mashabiki wakamatwe na Polisi kwa kuingia uwanjani wakiwa na jezi
hizo.
Lakini baadaye Polisi iliona hakuna kesi na kuifuta, baadaye Bin
Slum aliyemwaga Sh milioni 300 akiwa mfadhiri wa timu hiyo akajitokeza na
kupinga jambo hilo.
Hali iliyooonyesha kuudhi uongozi wa Coastal Union na kutangaza
kufungua kesi.








0 COMMENTS:
Post a Comment