MAKAMU Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Benjamin Kalume, ametaja majina ya wagombea waliopitishwa katika nafasi ya urais ndani ya shirikisho hilo.
Waliopita ni Evans Mgeusa, Hawa Mniga na Wallace Karia, huku Ally Mayay, Ally Saleh na Oscar Oscar wakiondolewa kwenye kinyang’anyiro hicho kwa kushindwa kukidhi kanuni ambazo zilikuwa zimewekwa.
Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Agosti 7, mwaka huu jijini Tanga ambapo mbali na nafasi moja ya urais, kuna nafasi sita za wajumbe wa kamati ya utendaji zitagombewa.
Kalume amesema kuwa wanasimamia haki na katiba ya TFF hivyo kwa sasa ni jukumu lao kubandika majina ya wagombea wote ili kujua waliopita kwenye mchujo wa awali.
Aliongeza kuwa ni ruksa kwa wagombea kuleta pingamizi lakini mapingamizi yao yawe na mashiko.
Sasa kilichobaki ni kumwaga mchanga kwenye ugali maana wao si wamekojolea mboga!!!!!
ReplyDeleteLIWWWALLO NA LLIWE!!!!! In Aggrey Mwanry's voice!!!!
Ht iweje hapa,, me naona karia njia nyeupeeeee kuongoza miaka mingine
ReplyDeleteMayay imekuwaje wamemwengua, hilo sio sahihi kwa afya ya uchaguzi. Sasa huyo mama ataleta ushindani gani kama sio sawa na uchaguzi wa kisiasa, kupita bila kupingwa
ReplyDeleteTazana taratibu na kanuni kama hanakidhi akae pembeni
DeleteTaratibu gani, mbona hazijasemwa
DeleteSoma vizuri
DeleteKaria anajitengenezea mazingira. Lakini kiongozi mzuri anatakiwa kushindana na ye yote na kushinda.
ReplyDeleteMshindani lazima awe na vigezo vilivyowekwa ndo wakina mwakalebela hao kuja kuleta matatizo wakipita
DeleteYaani hata huku nako tuumizane vichwa kudai uchaguzi huru na wa haki!!!Dawa ni kupelekana mahakamani tufungiwe na FIFA bila ya kujali ile slogan yao wanayosema eti tuangalie afya ya mpira maana ndio kichaka chao wanachojifichia labda watatambua kuwa watu wamechoka kufanywa wajinga...
ReplyDeleteWanaweweseka wakubebwa
DeleteKweli siasa ni nzur ila watu ndio wabaya yaan
ReplyDeleteWagombea walioenguliwa ni kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi zilizopo. Haya mambo ya kuanza kulalamika ni ujinga usiomithilika.
ReplyDeleteKanuni zipi hizo?
DeleteFuatilia vzr uchaguzi usidandie treni kwa mbele, soma kanuni usitake utafuniwe kila kitu
DeleteNashauri Mayay aende Mahakamani. Kwanini wamfanyie mizengwe?.
ReplyDeleteHatumtaki Karia.
ReplyDeleteMAYA JAMANI HANA ELIMU, NA KINGINE UYANGA UYANGA NAO SHIDA
ReplyDeleteNi nani kakwambia hana elimu? Uchaguzi ukiopita Mayayi alipitishwa na ndiye aliyeleta upinzani mkubwa zaidi. Yaani kipindi kile alikuwa na elimu, leo hana elimu, mmmmh! Au mnataka muendeleze kuendesha soka la Tanzania katika mtindo kama wa kesi za akina Bernard Mirison, eh?
DeleteWewe unayejiita SHAIBU inawezekana elimu aliyo nayo Ali Mayai ni zaidi ya kiwango chako cha elimu...
DeleteSoma kanuni usilete unazili wa kitopolo hapa
DeleteNdiyo maana sisi July ligi bado wakati wenzetu tayari Wana ratiba ya msimu ujao ni siasa xa kijinga tu mtu anaamua kujitengenezea maxingira yake karia kapewa kimvuli cha watu ili apite bila kupingwa duhhh
ReplyDeletetime will tell
ReplyDeleteMalipo ni hapa hapa duniani, Haiwezekani uchaguzi mkubwa kama wa tff, Fomu zitoke kwa siku nne tu, na zirudi zikiwa na wazamini,
ReplyDeletehapa imetumika kanuni, tar 8 ilitumika "tunasikitishwa"
ReplyDeleteNendeni FIFA mkashitaki
DeleteWe dada Ngosi acha kumshobokea bwana wako Karia,unajua asipopita na wewe maslahi yako yatakuwa yameenda na kura
Delete