Mshambuliaji wa Simba, Mkenya Paul Raphel
Kiongera, amefunguka kuwa pamoja na wao kushindwa kuibuka kidedea dhidi ya
Yanga, wachezaji wa timu yake walionyesha uwezo, hasa kipa kinda Peter Manyika
aliyehimili mikikimikiki ya wapinzani wao.
Kiongera alikuwa jukwaani akiwa na mwanaye
wanaishuhudia mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara.
Baadaye mshambuliaji huyo alisema alifuatilia
mchezo huo kwa umakini na ilikuwa ni mara yake ya kwanza kushuhudia Simba na
Yanga akiwa Tanzania, lakini aliridhishwa na kiwango cha wenzake ambao
walicheza.
Alisema timu yake isikate tamaa, zaidi iendelee
kujituma katika michezo ijayo kwa sababu walifanya kazi kubwa katika mchezo wa
juzi, hasa kipa ambaye ilikuwa mechi yake ya kwanza ya ligi.
“Kiwango walichokionyesha Simba kilikuwa
kizuri, walifanya kazi kubwa, japo walipoteza nafasi nyingi lakini Manyika
amefanya kazi nzuri katika mchezo wa juzi, ingawa ulikuwa na ushindani mkubwa,”
alisema Kiongera.
Kiongera kwa sasa anaendelea na matibabu, muda
si mrefu anaweza akarejea uwanjani na kuungana na timu yake baada ya maendeleo
yake kuwa mazuri.
0 COMMENTS:
Post a Comment