Siku chache baada ya Ndanda FC kumtupia virago kocha wake, Denis Kitambi, makocha wanne
wamejitokeza kuomba kazi ya kuifundisha timu hiyo akiwemo Mkenya mmoja.
Ndanda wameamua kuachana na
Kitambi kufuatia kufanya vibaya
katika mechi tatu mfululizo kwa kufungwa hivyo kujikuta ikiwa katika nafasi ya
12 ya msimamo wa ligi ikiwa na pointi tatu licha ya kuanza kwa kishindo katika
mchezo wa kwanza kwa kuifunga Stand United mabao 4-1.
Katibu wa Ndanda, Seleman
Kachele, amesema makocha wanne hadi sasa wamejitokeza kuomba kuifundisha timu
hiyo kwenye ligi huku wakitarajia
kupokea CV za makocha zaidi na kudai kuwa wapo katika mazungumzo nao ili kuweza
kupata yule atakayefaa kwa ajili ya kuifundisha timu hiyo.
Aidha, katibu huyo alieleza
kuwa kwa sasa timu hiyo ipo chini ya mkurugenzi wa ufundi wa Ndanda, Amini
Mawazo hadi hapo atakapopatikana kocha mpya wa kuiongoza.
“Kuna makocha wanne ambao
wameleta barua zao za kuomba kuifundisha Ndanda watatu kutoka ndani ya nchi na
mmoja kutoka Kenya.
“Tunaendelea kufanya nao
mazungumzo na wote wana leseni za Class A, hivyo ni matarajio yetu tutapata
kocha mzuri wa kuifundisha timu yetu kwani lengo letu ni kuhakikisha tunafanya
vyema kwenye ligi.
“Muda si mrefu tutamtangaza
kocha mpya mara baada ya kukubaliana naye,” alisema Kitambi.
0 COMMENTS:
Post a Comment