October 22, 2014


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kupitia Bodi ya Ligi limesema huenda likailima faini ya Sh 500,000 klabu ya Yanga kwa kitendo cha kususia kutumia chumba cha kubadilishia nguo katika mchezo wao dhidi ya Simba SC uliofanyika Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.


Katika mchezo huo Yanga hawakukitumia chumba hicho na badala yake kukitumia chumba cha mikutano na waandishi wa habari, huku kukiwa na tetesi kuwa waliamua kufanya hivyo baada ya kuwahisi wapinzani wao waliwafanyia vitendo vya kishirikina.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Silas Mwakibinga, alisema kuwa wamezisikia taarifa hizo ambazo kwao siyo rasmi hivyo wanasubiri ripoti ya mchezo huo ili kuijadili na kuitolea ufafanuzi.

Alisema kuwa sheria zinaonyesha wazi kuwa, iwapo Yanga itabainika kufanya kitendo hicho lazima ikumbwe na rungu hilo la faini kama sheria zinavyosema.


“Sheria zipo wazi na kama kweli walifanya hivyo lazima waadhibiwe, kabla ya wiki hii kumalizika kamati itakaa kuijadili ripoti ya mechi hiyo na faini ya shilingi laki tano itawakumba iwapo tutalikuta suala hilo,” alisema Mwakibinga.

1 COMMENTS:

  1. Hapo Yanga hawana cha kukwepa faini kwani hata Stand United walipigwa faini kwa jambo hilohilo kwa timu hiyihiyo ya Simba(Wanadai Simba hupuliza dawa ya kuchosha mwili chumba cha wapinzani wao sijuhi ni kweli!)

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic