Kocha Marcio Maximo amewaambia wachezaji wake kuwa sasa ataanza kazi kamili ya kuhakikisha wanaichapa Simba Oktoba 18.
Kocha huyo Mbrazil, ameonekana kuwa na furaha baada ya wachezaji wake kumaliza majukumu ya Taifa Stars ambayo iliitwanga Benin kwa mabao 4-0.
"Kocha amesema kwa kuwa wachezaji wote watakuwa nasi, itakuwa vizuri kwake kufanya vitu kwa pamoja.
"Hivyo ametutaka kuwa makini kumsikiliza, kuelewa na kutekeleza," alisema mmoja wa wachezaji wa Yanga.
Hivi karibuni, nusura Yanga itie ngumu kuwaachia wachezaji wake kwa ajili ya mechi hiyo ya kirafiki.
Maximo naye alikuwa mkali kuhusiana na hilo kwa kuwa lilikuwa linatibua programu zake hasa kutokana na wachezaji wake kuchukuliwa kwa muda mrefu.
Yanga inaendelea kujifua jijini Dar es Salaam wakati watani wao Simba wao wamepiga kambi jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini.
0 COMMENTS:
Post a Comment