MWAMWAJA. |
Kocha
Mkuu wa Prisons ya Mbeya, David Mwamwaja amesema hakutakuwa na kazi lahisi kwa
Simba.
Prisons
itakuwa mwenyeji wa Simba katika mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu Bara nje ya
Dar es Salaam katika msimu huu.
Tayari
Simba imecheza mechi nne na kutoka sare zote kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Mwamwaja
aliyewahi kuinoa Simba amesema kazi itakuwa ngumu na Simba isitarejie mteremko
hiyo wikiendi.
“Tumejiandaa
kwa kuwa tunataka kurekebisha makosa ya kufungwa na JKT.
“Tulicheza
vizuri katika mechi iliyopita, lakini si kwa kiwango cha juu sana. Sasa tunaweza
kuitumia nafasi ya kurekebisha makosa dhidi ya Simba,” alisema Mwamwaja mmoja
wa makocha wakongwe wazalendo.
Katika
mechi yake ya mwisho, Simba iliyotua mjini Mbeya jana ilitoka sare dhidi ya
Yanga wakati Prisons ilipoteza dhidi ya JKT Ruvu.
0 COMMENTS:
Post a Comment