BAADHI YA KOZI ZA MAKOCHA ZILIZOFANYIKA JIJINI DAR. |
Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania
(TOC) Gulam Rashid kesho (Oktoba 24 mwaka huu) atafunga kozi ya makocha ya
Leseni C ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Hafla ya ufungaji kozi hiyo
iliyoshirikisha makocha 32 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar na kuandaliwa na
TOC kupitia Olympic Solidarity kwa ushirikiano na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) itafanyika saa 5 asubuhi kwenye hosteli za TFF zilizopo Uwanja
wa Karume, Dar es Salaam.
Kozi hiyo ya wiki mbili iliyoanza Oktoba
12 mwaka huu iliendeshwa na Mkufunzi wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa
Miguu (FIFA) Ulric Mathiot kutoka Shelisheli.
Makocha walioshiriki kozi hiyo ni Ahmed
Suleiman Simba (Alliance), Akida Saidi (Lindi), Ally Bushir Mahmoud (Zanzibar),
Aloyce Akwilin (Pwani), Amin Rashid Mdowe (Zanzibar), Augustino Dakto Damian
(Katavi), Athuman Bilal (Shinyanga), Bakari Shime (Tanga), Charles Mayaya
(Shinyanga) na Choki Abeid (Geita).
Wengine ni Edna Lema (Morogoro), George
Melchior (Kagera), Godfrey Kapufi (Katavi), Hamis Mabo (Kigoma), Hawa Bajangero
(TWFA), Ibrahim Mulumba (Geita), Jemedari Said (TAFCA), Kenny Mwaisabula
(TAFCA), Madenge S. Omari (Mara), Milambo Camil (Tabora) na Mohamed D (Ruvuma).
Pia wapo Mohamed Ismail Laiser
(Manyara), Mohamed Muya (Dodoma), Ngawina Ngawina (Mtwara), Nicholas Kiondo
(Ilala), Osuri Charles Kosuri (Simiyu), Rachel Palangyo (TWFA), Salvatory
Edward (Temeke), Seif Bausi Nassor (Zanzibar), Yusuf Macho (Kigoma), Wilfred
Mollel (Iringa) na Zacharia Mgambwa (Rukwa).
Makocha watakaofaulu kozi hiyo watapewa
Leseni C za CAF wakati watakaoshindwa watapewa vyeti vya ushiriki tu.
0 COMMENTS:
Post a Comment