Kocha wa makipa anayewanoa Simba, Zdravko Djekic ametumia muda
mwingi kuwanoa makipa wa Casillas na Peter Manyika mambo mbalimbali, ikiwemo
namna ya kuthibiti mipira ya juu.
Katika mazoezi yanayoendelea kwenye kambi ya Simba jijini
Johannesburg, Djekic amekuwa akiwanoa makipa hao namna ya kuthibiti mipira ya
juu ambayo wakiiachia ni hatari kwa washambuliaji wa kupiga vichwa kama Jaja wa
Yanga.
Raia huyo wa Croatia amekuwa akiwaonyesha nini cha kufanya na
umuhimu wa kuiwahi kabla haijafika kwa mshambuliaji.
Kocha huyo amekuwa akiwanoa makipa hao baada ya Simba kumuacha
jijini Dar kocha wake wa makipa, Iddi Pazi ‘Fether’.
0 COMMENTS:
Post a Comment