October 15, 2014


Sergio Ramos, Filipe Luis na Joao Miranda ndiyo mabeki watatu ambao wanawania nafasi ya Beki bora wa La Liga 2014.

Sherehe za kuwakabidhi tuzo na kumtoa mshindi zitafanyika Oktoba 27.
Ramos ameingia kutokana na msaada wake kuisaidia Real Madrid kubeba Ligi ya Mabingwa Ulaya 'La Décima' na Kombe la Mfalme 'Copa del Rey'.
Amecheza mechi 32, amefunga mabao manne na pasi moja iliyozaa bao. Na ndiye anaishikilia tuzo hiyo.
Filipe Luis, sasa ni tegemeo kayika kikosi cha Atletico Madrid, amecheza dakika 2,880 msimu uliopita.
João Miranda ndiye anafunga watu hao watatu wa mwisho wanaowania tuzo hiyo.
Ameisaidia Atletico Madrid kutwaa Kombe la La Liga na Super Cup, anasifika kuongoza ulinzi imara.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic