KITAMBI: ALIIPANDISHA NDANDA FC, IKAANZA NA USHINDI LIGI KUU IKIWA UGENINI SHINYANGA. |
Ndanda FC imemfuta kazi
kocha wake, Denis Kitambi.
Taarifa zilizoifikia
SALEHJEMBE zinaeleza, uongozi wa klabu hiyo umechukua uamuzi huo baada ya
vipigo viwili dhidi ya Mtibwa Sugar na kile cha nyumbani jana dhidi ya Ruvu
Shooting.
Taarifa nyingine zimeeleza kuwa Kocha wa Makipa, Mohammed Mwarami 'Shilton' naye ametimuliwa pia.
Imeelezwa kumekuwa na kikao cha dharura leo asubuhi na viongozi wamefikia uamuzi huo.
Juhudi za kuwapata viongozi
wa Ndanda FC zimekuwa zikikwama kutokana na viongozi hao kutopokea simu.
Lakini mchezaji mmoja wa
Ndanda FC amelithibitisha hilo.
“Tumeambiwa kuwa wamemtimua
kocha, ila bado viongozi hawajafika kutueleza,” alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment