Kocha wa Mwadui, Jamhuri Kihwelo 'Julio' amesema wataendelea kupambana katika Ligi Daraja la Kwanza licha ya kutokuwa na mwanzo mzuri.
Julio amesema anajua sare mbili na kipigo kimoja, kinaashiria ligi hiyo si lelemama.
"Hata ukiangalia, walioshinda wengi ni bao moja au mbili moja. Hii inaonyesha ligi hii ni ngumu.
"Tunalijua hilo, ila tutaendelea kupambana kuhakikisha tunafanya vizuri katika mechi nyingine.
"Tulicheza mechi zote nje ya nyumbani sasa tunanza na Polisi Mara, hii haina maana mechi itakuwa lahisi, lakini tutapambana kushinda," alisema Julio.
Kikosi cha Mwadui chenye wachezaji wakongwe kama Mohammed Banka, Bakari Kigodeko, Juma Jabu na wengine, kilipoteza dhidi ya Toto kabla ya kutoka sare mbili.
Mechi inayofuatia ni dhidi ya Polisi Mara na itapigwa kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment