October 11, 2014


Kocha Patrick Phiri ameamua kuongeza dozi ya kikosi chake baada ya kugundua mambo kadhaa ambayo ameyaona kasoro.

Simba iko jijini Johannesburg ambako imeweka kambi kujiandaa na mechi ya Oktoba 18 dhidi ya Yanga, pamoja na Ligi Kuu Bara.
Kikosi cha Simba sasa kitakuwa kikifanya mazoezi mara mbili kwa siku yakiwemo yake ya nguvu.
"Kweli kocha ameona pia kulikuwa na tatizo la stamina, hivyo kutakuwa na mazoezi magumu kidogo.
"Sasa tutafanya mara mbili kwa wiki, lakini siku za mechi kama Jumamosi (leo) hakutakuwa na mazoezi, tutapumzika tu," kilieleza chanzo kutoka Afrika Kusini.
"Kocha kasema hatuna stamina, lakini kuna mambo mengine amekosoa, hivyo tunayafanyia kazi pia ili tukirejea, tuwe fiti kabisa."
Simba imeanza Ligi Kuu Bara kwa sare tatu mfululizo, hali ambayo imezua hofu kwa uongozi wa klabu hiyo pamoja na mashabiki wake.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic