Polisi 400 watakuwa na jukumu la kufanya ulinzi wakati wa pambano
la Ligi Kuu Bara litakalowakutanisha watani Yanga na Simba.
Pambano hilo litachezwa Jumamosi na kuwakutanisha Yanga na Simba
ambao kila upande wameingia kambi.
Ofisa Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Silas Mwakibinga amesema hilo
wamehakikishiwa na Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam.
“Kweli, polisi ni mia nne. Hivyo tuna uhakika wa suala la ulinzi,”
alisema.
“Tunawaomba mashabiki kuwa watulivu katika mechi hiyo ili tuweze
kushuhudia burudani nzuri,” alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment