Rais wa Simba, Evans Aveva amesema vipigo viwili walivyovipata
Simba nchini Afrika Kusini, vimewapa funzo na kumsaidia Kocha Patrick Phiri.
Aveva amesema mashabiki wa Simba wanapaswa kukubali kambi ya
Afrika Kusini ilikuwa ni kwa ajili ya mafunzo.
“Kufungwa mechi mbili imemsaidia mwalimu kuangalia mambo ambayo
yanaweza kuwa tatizo.
“Tulianza ligi kwa kutoka sare mechi zote tatu, kambi ya Afrika
Kusini ilikuwa ni kwa ajili ya kujiimarisha ili kufanya vizuri kwenye ligi na
mechi zote za ligi,” alisema Aveva.
Simba ikiwa Afrika Kusini ilianza kwa sare ya bila kufungana dhidi
ya Orlando Pirates kabla ya kutwangwa mabao 4-2 dhidi ya Wits na Jomo Cosmos
wakawafunga 2-0.
Tayari Simba imerejea jijini Dar es Salaam na kuweka kambi jijini
Dar es Salaam.
Simba ilianza ligi kwa sare tatu mfululizo dhidi ya Coastal Union,
Polisi Moro na Stand United.
0 COMMENTS:
Post a Comment